Taarifa maalumu kwa wanafunzi wote.
Imetokea kuwa ni mazoea kwa wanafunzi kutozingatia sheria za chuo na hivyo kupunguza ufanisi katika masomo yao. chuo kinapenda kuwakumbusha na kuwatahadhalisha wanafunzi wote kuhusiana na ufuatwaji wa sheria za chuo. kuna baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakichelewa kufika madarasani na katika vyumba vya kufanyia mitihani. chuo kinapendekeza adhabu kali zitolewe na walimu kwa mwanafunzi yeyote atakekiuka sheria za chuo. kwa mfano mwanafunzi atakapochelewa kuingia darasana zaidi ya dakika 15 azuiliwe kuingia darasani na pia katika mitihani ya ngazi zozote zile itakayo fanyika hapa chuoni kama mwanafunzi atachalewa kuwasili zaidi ya dakika 30 basi azuiliwe kufanya mtihani huo. Kwa utaratibu huu wanafunzi na walimu wao watafanikiwa katika kuimarisha nidhamu ya masomo kwa wanafunzi na kuboresha maendeleo ya elimu kwao.
Imetolewa na Mkuu wa chuo
Lisbon Business College
Hili ni jambo la muhimu na la kuzingatiwa na pande zote kutoka kwa wanafunzi lakini pia kwa walimu.
ReplyDelete